Email Us

MINISTRY OF HEALTH

NATIONAL PUBLIC HEALTH LABORATORY

ISO 15189:2012 ACCREDITED

TRAINING ON BIOSAFETY AND BIOSECURITY

Posted on: March 11th, 2026

Wizara ya Afya kupitia Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii (NPHL)kwa kushirikiana na African CDC, chini ya Kituo cha Kikanda cha Umahiri cha ulinzi na usalama wa kibaiolojia (RCoEBB) – Tanzania, wanaendesha Mafunzo ya Kikanda ya Uteuzi, Ufungaji, Matengenezo na Uthibiti ubora  wa Makabati ya Usalama wa Kibailojia (BSCs) yaliyoanza leo tarehe 02 Machi 2026 na kumalizika tarehe 13 Machi 2026.

Mafunzo haya yanalenga kujenga uwezo wa wataalamu kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, zikiwemo South Sudan, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Comoros, Mauritania, Djibouti, Uganda, Somalia, Madagascar na Tanzania, katika usimamizi, ugezi na matengenezo kinga  ya makabati ya usalama wa kibailojia.

 Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa, Bw. Ambele Mwafulango, akifungua mafunzo hayo alisisitiza kuwa jitihada hizi za pamoja zinazoongozwa na Africa CDC zinalenga kuhakikisha maabara zetu zinafikia viwango vya ulinzi na usalama wakibaiolojia kimataifa.

Aidha, alibainisha kuwa: “Hatufundishi tu ufundi wa vifaa tiba; tunajenga msingi wa umahiri na usalama unaoaminika barani Afrika na duniani kote.”


                 












LOCATION

ADVERT

image description

VIDEO GALLERY

Contact Us

  • Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii
  • EPZA area,mandela road
  • S.L.P 9083, Dar Es Salaam
  • Telephone: +255 734 677 337
  • Mobile: +255 734 677 338

Visitors Counter

  • Today 282
  • Yesterday 489
  • This Week 1647
  • This Month 3034
  • All Days 84199
@ NPHL.All Rights Reserved
@ Developed By NPHL & MOH Team
}