Email Us

MINISTRY OF HEALTH

NATIONAL PUBLIC HEALTH LABORATORY

ISO 15189:2012 ACCREDITED

UFUNGUZI WA MAABARA YA TAIFA YA AFYA YA JAMII KUWA KITUO CHA KIKANDA CHA AFRIKA MASHARIKI CHA MAFUNZO YA ULINZI NA USALAMA WA VIMELEA

Posted on: April 3rd, 2023


Serikali itaendelea kuboresha huduma za Maabara zote nchini kwa kuzingatia matakwa ya ulinzi na usalama wa Kibiololia na kuhakikisha usalama wa watenda kazi pamoia na mazingira yote kwa ujumla. Hayo yamesemwa leo Aprili 3, 2023 na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa hafla ya ufunguzi wa Maabara ya Taifa va Afya ya Jamii kuwa kituo cha Kikanda cha Afrika Mashariki cha Mafunzo ya ulinzi na usalama wa vimelea jijini Dar es Salaam. Waziri Ummy amesema kuwa Serikali inafanya juhudi mbalimbali za kuhakikisha usalama wa afya za Watanzania na wote waishio ndani ya mipaka ya Tanzania inalindwa. "Wizara inatekeleza viwango vya Kitaifa na Kimataifa kuhakikisha vimelea hatarishi vinavyotokana na hatua za upimaji na tafiti ndani ya maabara havisambai katika jamii  na kuleta madhara kama vile milipuko ya magonjwa". Amesema kuteuliwa kwa kituo hicho kunadhihirisha jinsi maabara ya Taifa ya Jamii inaendelea kuaminika duniani na kuwa na uwezo wa kupima vimelea vyote hatarishi kwa kuwa vimelea hatarishi vinaweza kutoka kwa wanyama kwenda kwenye mazingira na baadaye kuathiri afya ya binadamu. Aidha, Waziri Ummy amesema tangu kutangazwa kwa kituo hicho wamekwishapokea maombi toka Chuo Kikuu cha Musinde Murilo chini Kenya ya kuleta wanafunzi wanaochukua shahada ya ulinzi na usalama wa vimelea kwa ajili ya elimu kwa vitendo na kudhihirisha kwamba maabara inaaminika na inayo uwezo. Naye, mwakilishi kutoka Afrika CDC Dkt. Talkmore Maruta ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini va uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwazi wa kutoa taarifa hususani ya ugonjwa wa Marburg na hivyo kuonesha namna nchi inakuwa salama na kuongeza kuwa CDC itaendelea kushirikiana na Serikali na kuwaiengea uwezo wataalamu wa afya chini katika kujiandaa, kutambua na kukabiliana na magonjwa ya milipuko.

LOCATION

ADVERT

image description

VIDEO GALLERY

Contact Us

  • Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii
  • EPZA area,mandela road
  • S.L.P 9083, Dar Es Salaam
  • Telephone: +255 734 677 337
  • Mobile: +255 734 677 338

Visitors Counter

  • Today 65
  • Yesterday 269
  • This Week 954
  • This Month 522
  • All Days 30060
@ NPHL.All Rights Reserved
@ Developed By NPHL & MOH Team
}