Email Us

MINISTRY OF HEALTH

NATIONAL PUBLIC HEALTH LABORATORY

ISO 15189:2012 ACCREDITED

Regional Training on Biosafety & Biosecurity

Posted on: May 14th, 2026

Wizara ya Afya kupitia Kituo cha Umahiri cha Kikanda cha Usalama wa Vimelea na Ulinzi Dhidi ya Vihatarishi vya kibaolojia Tanzania (RCoEBB) kilichopo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii (NPHL), imefungua rasmi mafunzo ya kikanda kuhusu Biocontainment yanayofanyika kuanzia tarehe 11–15 Mei 2026.

Mafunzo hayo yanawakutanisha washiriki kutoka nchi wanachama wa Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Somalia, Sudan Kusini, Madagascar, Mauritius, Comoro na Tanzania pamoja na taasisi washirika na wataalamu wa afya ya umma.

Lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha uwezo wa kikanda katika maeneo ya biosafety, biosecurity, usalama wa maabara, tathmini ya vihatarishi na maandalizi ya dharura kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.

Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Maabara ya Taifa, Bw. Ambele Mwafulango, aliwataka washiriki kutumia nafasi hiyo kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika kuimarisha usalama wa afya ya jamii.

Mafunzo hayo yanaakisi dhamira ya Tanzania katika kuimarisha usalama wa afya ya jamii na mifumo ya kukabiliana na vihatarishi vya kibaolojia katika ukanda wa Afrika Mashariki





LOCATION

ADVERT

image description

VIDEO GALLERY

Contact Us

  • Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii
  • EPZA area,mandela road
  • S.L.P 9083, Dar Es Salaam
  • Telephone: +255 734 677 337
  • Mobile: +255 734 677 338

Visitors Counter

  • Today 216
  • Yesterday 271
  • This Week 1429
  • This Month 4458
  • All Days 101279
@ NPHL.All Rights Reserved
@ Developed By NPHL & MOH Team
}