MINISTRY OF HEALTH
NATIONAL PUBLIC HEALTH LABORATORY
ISO 15189:2012 ACCREDITED
KAMATI YA BUNGE YA AFYA NA MASWALA YA UKIMWI YATEMBELEA OFISI ZA MAABARA YA TAIFA YA AFYA YA JAMII ZILIZOPO MABIBO JIJINI DAR ES SALAAM
Posted on: September 14th, 2023
Kamati ya Bunge ya Afya na maswala ya Ukimwi ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Stanslaus Nyongo, imetembelea Ofisi za Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii kuona Mpango na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Maabara hiyo.Kamati hiyo ya Bunge kwa pamoja imefurahishwa sana na juhudi za Maabara ya Taifa kuwa mstari wa mbele katika kuisaidia wizara ya Afya na serikali katika kupambana na Magonjwa ya mlipuko kama COVID19, Marburg n.k
Kaimu Mkurugenzi wa Maabara, Mr. Medard Beyanga akiielezea Kamati hiyo baada ya kuitembeza kwenye vitengo mbalimbali ndani ya ofisi za Maabara, alielezea malengo mikakati na kazi kuu zinazofanywa na Maabara ambapo alifafanua kuwa kazi hizo ni pamoja na rufaa ya sampuli za vimelea hatarishi (referral Laboratory for High pathogenic samples), utambuzi na uthibitisho wa magonjwa ya mlipuko, ufuatiliaji wa magonjwa (Disease Surveillance), kuandaa na kusambaza sampuli za ubora.
Mkurugenzi alifafanuwa kuwa wakati wote Maabara imejiandaa kukabiliana na Magonjwa ya mlipuko ambapo alitolea mfano namna wataalamu wa Maabara ya Taifa walivyo fanya juhudi kupambana na ugonjwa wa Marburg huko kagera ambapo ugonjwa huo ulitangazwa kuisha na Waziri wa Afya Mhe. Ummy mwalimu mnamo 02 Juni 2023.
Aidha, Mkurugenzi aliielezea Kamati hiyo ya Bunge kuwa Maabara ya Taifa ina Maabara jongezi (Mobile Lab) zinazotumika katika kupambana na magonjwa ya mlipuko. Moja kati ya mafanikio makubwa ya Maabara ni pamoja na kuteuliwa kuwa kituo cha kikanda cha mafunzo ya ulinzi na usalama wa vimelea.
Contact Us
- Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii
- EPZA area,mandela road
- S.L.P 9083, Dar Es Salaam
- Telephone: +255 734 677 337
- Mobile: +255 734 677 338
Related Links
Useful Links
Visitors Counter
- Today 69
- Yesterday 269
- This Week 956
- This Month 525
- All Days 30061